Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewainua Wabunge na Wageni waalikwa Bungeni kusimama kwa dakika moja kwa ajili ya kuwaombea waliopoteza maisha kwenye maandamano ya october 29,2025 ambapo ametoa pole kwa waliofariki, kujeruhiwa na kupoteza mali na amesema Serikali imeunda Tume ya kuchunguza yaliyotokea.
Rais Samia amesema “Mimi binfasi nimehuzunishwa sana na tukio lile natoa pole kwa Familia zote zilizopoteza Familia zao tunaomba waliofariki wapumzishwe kwa amani, kwa majeruhi tunawaombea wapone haraka na waliopoteza mali zao tunawaomba wawe na ustahimilivu”
“Serikal imeunda Tume ya kuchunguza yaliyotokea ili tujue kiini cha tatizo taarifa hiyo itatuongoza kujielekeza kwenye mazungumzo ya kuleta maelewano na amani” ——— Rais Samia Bungeni leo.