Jihadhari na uwovu huu

Comentarios · 25 Puntos de vista

Mbinu mpya inayotumika na majanbazi

Habari zenu nyote.

 

Mimi na familia yangu tulishuhudia jambo fulani kupitia dirishani kwetu kati ya saa 7:30 na saa 8:45 usiku wa kuamkia leo, hivyo nimeamua kulishirikisha ili sote tuwe waangalifu.

 

Kuna mtu aliacha kwa makusudi mtoto mchanga aliyekuwa amefungwa kwa kitambaa cheupe mbele ya geti letu. Mtoto huyo alilia kwa zaidi ya dakika 30 kisha akanyamaza. Baadaye, mwanaume mmoja aliyekuwa amevaa nguo nyeusi na kujificha nyuma ya ukuta wetu alitambaa hadi alipokuwa mtoto huyo na kumpiga tena ili aanze kulia.

 

Alipoona hakuna mtu anayefungua mlango wala kutoka kuangalia mtoto huyo, alitoka mafichoni, akambeba mtoto na kumhamisha kutoka barabarani. Dakika chache baadaye, teksi ilifika na wakaondoka.

 

Tulimpigia simu jirani yetu na kumuuliza kama amewahi kuona jambo kama hilo karibu na nyumba yake. Alituambia kuwa hii ni mbinu mpya inayotumiwa na majambazi wenye silaha ili kuwavuta watu watoke nje ya nyumba zao na kisha kuwapora. Alisema kaka yake mkubwa aliporwa wiki iliyopita kwa kutumia mbinu hiyo hiyo.

 

Tafadhali tuwe macho na waangalifu. Wajulishe marafiki na familia zenu. Asanteni.

C&P

Comentarios