2 d - Vertalen

Watu wengi sana ambao nimekutana nao wanaoitwa KICHWA CHA FAMILIA...

Au WANAOONEKANA ndio msaada Mkubwa kwenye familia zao, huwa wanapitia MAMBO MAGUMU sana na hawana mtu wa KUWASIKILIZA.

Wengi huwa wanatumia sehemu KUBWA ya KIPATO chao kusaidia ndugu zao.

Wengi huwa hawaishi maisha wanayotamani kwa sababu WANAJITOA sana kusaidia ndugu zao.

Wengi wao huwa WANALAUMIWA sana wanaposhindwa kufanya kitu bila kujali hali zao na HUWA watu wanasahau kujitoa kwao kwa kila siku.

Wengi hujikuta wakiwa na MSONGO mkubwa wa mawazo na HAKUNA anayewajali au kuwasikiliza.

Wengi wameingia kwenye MADENI kwa sababu walikuwa wanatafuta pesa ili kusaidia shida za ndugu zao.

Wengi huwa wanachelewa kuwa na MAENDELEO BINAFSI kwa sababu wanatumia PESA zso nyingi kwa ajili ya NDUGU.

Wengi huwa WANAUMIZWA sana na MANENO ya ndugu au KUSALITIWA na ndugu waliowahi kuwasaidia.

Wengi wao huwa ni watu wenye HUZUNI za muda mrefu na wakiwa peke yao huwa ni watu wa KULIA na MACHOZI kwa sababu ya MZIGO MZITO waliobeba.

Wengi wanajinyima ndani ya FAMILIA zao na WATOTO na WENZI wao huwa wanalipa GHARAMA wanazobeba.

Bahati mbaya sana, siku wakiwa kwenye SHIDA au WAKIFA, hakuna anayekumbuka MKE/MUME au WATOTO WAKE.

Kama una mtu kama huyu kwenu, leo mtafute mpigie simu/mtumie meseji au hivi karibuni mtembelee na UMSHUKURU na KUMTIA MOYO, utakuwa umemuongezea NGUVU SANA.

Wengi hawawezi KUSEMA ila wanahitaji FARAJA sana.

Kama umependa makala hii tafadhali share na wengine.

See You At The Top