Share na Kwa mpambanaji mwingine apate ujumbe huu
Mwambie huyo anayekuharibia mipango yako kitu kimoja tu ЁЯСЗЁЯП╛
Kua
Mimi sina ndoto za kuwa daktari.
Sina ndoto za kuwa engineer.
Sina ndoto za kuwa mbunge, waziri wala rais.
Sina mpango na cheo chochote kikubwa cha sifa na makofi.
Mimi napambana kwa ajili ya kitu cha msingi kuliko hivyo vyote тАФ
NAFUTA NJAA NYUMBANI.
Unapoharibu mishe zangu,
huharibu jina languтАж
unahatarisha sahani ya chakula cha watoto wangu.
Unapozuia riziki yangu,
hupigi vita ndoto zanguтАж
unapiga vita familia yangu.
Kuna watu wanapambana kwa ajili ya umaarufu,
lakini kuna wanaume wanapambana kwa ajili ya bili za umeme, kodi ya nyumba na ada ya watoto.
Heshimu jasho la mtu.
Kama huwezi kusaidia, usiharibu.
Maana wengine hatutafuti vyeo тАФ
tunatafuta mkate wa kila siku.
Dismas Mato
#jeshi_ya_allah