6 w - Traduire

๐‡๐€๐’๐ˆ๐‘๐€: ๐Œ๐จ๐ญ๐จ ๐”๐ง๐š๐จ๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐Š๐ฎ๐œ๐ก๐จ๐ฆ๐š ๐Œ๐š๐ข๐ฌ๐ก๐š ๐˜๐š๐ค๐จ ๐๐๐š๐ง๐ข ๐ฒ๐š ๐’๐ž๐ค๐ฎ๐ง๐๐ž ๐‚๐ก๐š๐œ๐ก๐ž

Watu wengi wanaharibu vitu muhimu maishani si kwa sababu walitakaโ€ฆ bali kwa sababu ya sekunde chache za hasira.

Hasira ni kama moto. Ikianza kuwaka, haiulizi inachoma nini. Inaweza kuchoma maneno yako, mahusiano yako, heshima yako, hata fursa ambazo zingebadilisha maisha yako. Tatizo ni kwamba watu wengi hutambua uharibifu baada ya moto kuzimika.

Dakika chache za hasira zinaweza kugharimu miaka ya kujenga uaminifu. Neno moja la hasira linaweza kuacha kovu la kudumu kwenye moyo wa mtu mwingine.

Ndio maana watu wenye hekima hawapigani na hasira kwa nguvuโ€ฆ wanaisimamia kwa utulivu. Wanajua kuwa kabla ya kuchukua hatua, ni lazima kwanza watulize akili zao.

Ukipata hasira, simama kidogo. Vuta pumzi. Tafakari. Jiulize: โ€œJe, nitakayofanya sasa yatajenga au itaharibu?โ€

Watu wengi wanajuta baada ya hasira kupita. Wenye busara hujifunza kuitawala kabla haijaharibu kila kitu.
Usiruhusu sekunde za hasira ziharibu miaka ya juhudi zako.

๐Ÿ‘‰Usikose post kama hii โ€” bonyeza follow @fikrachanya_tz sasa hivi.
.
.
.
.
#hekimazamaisha #ukwelimchungu #fikrachanya #maishahalisi #jitambue

image