3 د - ترجمه کردن

Faida ya mlonge

🔵 Mti wa Mlonge husaidia waathirika wa H.I.V kuongeza cd4 cell (white blood cell) ndani ya
mwili ambayo humsaidia mgonjwa kuondokana na miwasho katika damu na
kuupa mwili nguvu na kuongeza hamu ya kula

🔵 Mti wa Mlonge hutibu maradhi sugu kama vile Kisukari (Kuimarisha na kurekebisha
Kiwango cha sukari katika mwili wa mwanadamu), Pressure, malaria, homa ya mara kwa
mala, saratani ya tumbo, hupunguza stress, huleta hamu ya kunywa maji, jambo
amabalo ni adimu kwa watu wengi pia huondoa uchovu mwili na kukufanya uwe na afya nzuri,
mchangamfu na mwenye furaha

🔵 Majani na maua ya Mlonge yana virutubisho vingi kama vitamin A (mara tatu zaidi
ya karoti), Vitamini C (mara tatu zaidi ya ile ya machungwa), calcium(mara 140 zaidi ya
ile inayopatikana katika maziwa ya Ng’ombe) na Potasiamu. Mmea huu umetumika
kusadia udhibiti wa matatanisho yanayoletwa na ugonjwa wa ukimwi

🔵 Faida nyingine itokanayo na unga wa majani ya mti wa mlonge ni kusafishia maji ambayo
ni machafu na kuweza kuwa safi na salama na kuwa tayari kwa matumizi yoyote ya
nyumbani kama vile kupikia na kunywa hii inaweza kuwa ni mbadala ya madawa
mengine yanayoweza kutibu maji kama vile watergard na mengineyo

🔵 Majani ya Mlonge yamepachikwa jina la chakula chenye viwango kwa sababu
wanasayansi waligundua yana kiasi cha madini ya Kalisium yanayoweza kupatikana katika
glasi nne za maziwa, kiasi cha vitamini c inayopatikana kwenye machungwa saba, Potasium
ya kwenye ndizi mbivu tatu. Pia unapata kiasi cha madini ya chuma mara nne zaidi

🔵 Majani ya Mlonge yana Vitamin A nyingi kuliko karoti, vitamin C nyingi kuliko machungwa
na madini ya Potassium nyingi kuliko ndizi mbivu, halikadhalika ubora wa protini yake ni
bora kushinda maziwa na mayai

🔵 Kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya chuma (Iron), kasiamu (Calcium) na
vitamin nyingi za aina mbalimbali, majani ya mmea huu yamekuwa yakitumika kama ‘tonic’
kwa watoto wadogo na vijana ili kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.

🔵 Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi. Waweza kutumia majani kama unavyotumia mchaichai na hapo unatibu MALARIA
bila kujua.
Majani ya Mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga.
Unga wake unaweza kuhifadhiwa kwa
muda mrefu bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi (zingatia usikaushe kwenye JUA)
Mafuta kutoka kwenye mbegu
za mti wa mlonge huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba.
Pia hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo.
Mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa

🔵 Licha ya kuwa dawa nzuri sana ya kusafisha tumbo (Jaribu kutafuna mbegu zake tatu baada ya
kumenya huku ukinywa maji mengi sana.
Mbegu za mti wa Mlonge ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi.
Pia mbegu hutumika katika kusafisha au kuchuja maji ambapo hupondwa na kuwekwa kwenye maji

🔵 Unga wa mizizi ya mlonge ukichanganya na unga msamitu husaidia haraka sana kwa wanaume wanaowahi kufika kileleni, wanaume walioathirika na madhara ya kujichua/punyeto. Unga huo ukichanganya tumia kunywa kijiko kimoja cha chakula kutwa mara mbili, changanyia kwenye maji ya uvuguvugu. Haya matumizi pia ndo utakayoyafanya unapotumia unga wa majani ya mlonge

🔵 Mmea wa Mlonge ndio mmea ulio na kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye manufaa kwa mwili wa binadamu na mifugo. Una virutubisho zaidi ya 90 na unaweza kutumiwa na watu wa umri wote Hakuna Madhara yoyote ya kutumia Mlonge ambayo yamethibitishwa na wataalamu, hivyo tumia mlonge kadri uwezevyo, hakikisha tu umeandaa vizuri.

image